Pengine miaka mitano mbele pale Canada kutakua na Umaskini mkubwa watu watalalamika hatuna shule hatuna meya wa jiji, hatuna maji safi, hatuna ajira, hatuna mabasi ila mwisho wa siku watasema haya yote kwetu hayana maana kwa sababu tuna kijana wetu Alphonso Davies hana uwezo wa kutupatia mahitaji haya bali anatufurahisha akiwa uwanjani. hivyo tumaini letu la kesho lipo kwenye Ubongo na Miguu yake.
Alphonso Davies
Alphonso Davies

Ni kama ule mto Nile wa pale kwa Mafarao maji yake yanayochuruzika, Anashuka tu, Anamwagika tu, Anamiminika tu, Kama una kiu ya soka basi maji yanapatikana mguuni mwake. Kama unaugua soka tiba ipo mwilini mwake.

Kama Kuna jambo ambalo Bwana Hasan Salihamidzic hataki kulisikia hata kidogo na litamkera ni kukaa kwenye meza moja na Mafya yoyote kwenye soko la Ulaya ili atoe bidhaa itwayo Alphonso Davies .

Alimuliza maswali Mengi Kijana Raphinha na ikashindikana , kukosekana kwa majibu ikapelekea ujumbe ufike kwa Xavi kwakua mwalimu aliamua kumtumia Mwanafunzi wake imara Ochu ili akajibu pia ikashindikana .

Alphonso Davies, Alphonso Davies: Kijana Mkimbizi Anaeibeba Bayern Munich Mabegani, Meridianbet
Alphonso Davies

Yes Kama Jose anafurahi kila akiona timu ina moyo wake kwa sababu ni muhimu zaidi . Basi miyoyo inayotakiwa kwenye timu ndio hii inakupa uwiano sawa wakati wa kijilinda na kushambulia bila ya kupungua ufanisi wowote kwenye kila tendo wakati mpira upo mguuni ama haupo.


Kwa habari na matukio ya kimichezo na ya uhakika tembelea Youtube channel yetu Meridian Sport

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa