Nyota wa Manchester United, Amad Diallo, amefunguka kuhusu maisha chini ya kocha wa muda Michael Carrick, akieleza kuwa wachezaji wa klabu hiyo wameridhishwa na uongozi wake na wangependa aendelee kuwa kocha mkuu msimu ujao.
Akizungumza Diallo amesema mabadiliko makubwa yameonekana ndani ya timu tangu Carrick aingie madarakani. Alisem “Nadhani mabadiliko makubwa ni kwa sababu timu sasa ina nguvu zaidi na inacheza kwa ushawishi mkubwa uwanjani.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Diallo aliongeza kuwa umoja wa chumba cha kubadilishia nguo umeimarika sana chini ya Carrick. “Ndani ya dressing room tuko pamoja sana, kosa la mmoja ni kosa la wote. Hatujali sana makosa, tunaendelea mbele kama timu inayotaka kushinda pamoja,” alifafanua.
Akizungumzia mustakabali wa kocha huyo, Diallo alionekana wazi kumunga mkono Carrick. “Kila mtu anafurahi kuwa naye kama kocha. Kila mmoja yuko pamoja naye,” alisema.
Aidha, alisisitiza kuwa wachezaji wote wangependa kuona Carrick akiendelea kuinoa Manchester United. “Tutafurahi sana kama tutakuwa naye msimu ujao kama kocha mkuu,” alisema kwa msisitizo.
Kauli hiyo imezidi kuongeza mjadala ndani ya klabu hiyo kuhusu hatma ya benchi la ufundi, huku mashabiki wakisubiri uamuzi wa uongozi wa Manchester United kuhusu nafasi ya kocha huyo baada ya mafanikio ya hivi karibuni.


