Kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti, amesema ana matumaini makubwa ya kumtumia nyota wake Neymar katika mchezo muhimu wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Scotland baada ya mshambuliaji huyo kuendelea vizuri na matibabu ya majeraha yake ya misuli ya mguuni.
Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Haiti, Ancelotti alifichua kuwa Neymar yuko katika hatua za mwisho za kurejea uwanjani. “Neymar atafanya mazoezi binafsi kesho na Jumatatu atajiunga na wachezaji wengine wa timu. Atakuwa tayari kwa mchezo dhidi ya Scotland,” alisema kocha huyo raia wa Italia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Neymar mwenye umri wa miaka 34 hajacheza tangu Mei 17 alipokuwa akiichezea Santos kutokana na majeraha ya misuli. Licha ya kukumbwa na majeraha katika kampeni ya kufuzu michuano ya Dunia 2026, bado alikuwa na mchango mkubwa kwa Brazil akifunga mabao mawili na kutoa pasi tatu za mabao katika mechi nne alizocheza.
Wakati huo huo, Ancelotti hakutaka kuthibitisha kama Matheus Cunha ataendelea kuanza katika nafasi ya mshambuliaji wa kati baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Haiti. “Inawezekana. Nafikiri Matheus alicheza vizuri katika nafasi hiyo na aliwasumbua mabeki wa wapinzani. Alitoa pasi nzuri na alikuwa na ufanisi mkubwa eneo la ushambuliaji,” alisema.
Brazil inaongoza Kundi C kwa pointi nne, ikilingana na Morocco lakini ikiwa mbele kwa tofauti ya mabao. Hata hivyo, Ancelotti amesema lengo lake si kuiondoa Scotland bali kuendelea kuboresha kiwango cha timu yake. “Hatufikirii kuhusu kuiondoa Scotland. Tunafikiria kucheza vizuri zaidi na kuendelea kuimarika. Scotland inaweza kutusumbua kama ilivyoisumbua Morocco, hivyo tunapaswa kuwa makini, watulivu na kujiandaa vizuri kwa mchezo huo,” alisisitiza.


