Anchelotti kocha wa klabu ya Real Madrid ameeleza kua mshambuliaji wake mahiri Karim Benzema anaweza kurejea kwenye mchezo wa dabi kati yao na Athletico Madrid siku ya jumamosi lakini kutakua hakuna hatari ya kuongezeka majerha ya kwa mshambuliaji huyo.

Real Madrid ambao walishinda mchezo wao wa mwisho kwenye ligi kuu ya Hispania dhidi ya Real Mallorca bila uwepo kwa mshambuliaji huyo tegemezi kwenye timu hiyo.

anchelottiCarlo alipoulizwa na wanahabari kuhusiana na hali ya mshambuliaji huyo kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabimgwa barani dhidi ya Rb Leipzig alisema “Anaendelea vizuri na anaweza kurejea katika mchezo wa dhidi ya mahasimu wao ndani ya jiji la Madrid kama tu kutakua hakuna hatari ya kupata majeraha zaidi”.

Mshambuliaji huyo alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhdi ya klabu ya Celtic ya Uskochi jumanne iliyopita ambao umemueka nje mpaka wakati huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa