Janne Andersson ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa Sweden amesema kwamba Zlatan Ibrahimovic lazima adhihirishe kuwa anataka kurudi tena kuichezea Sweden.

Mchezaji huyp mwenye umri wa miaka 39 hivi karibuni ameonekana kuwa tayari kurudi katika timu ya taifa baada ya kupost picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa ameweka ujumbe: “Muda mrefu sijawaona”.

Lakini, Andersson anaonekana kutomzingatia baada ya mapema mwezi huu kumuacha Ibrahimovic katika kikosi kipya cha Sweden na kusema kwamba: “Milango imefungwa”.

Ikiwa Ibrahimovic kuwa katika fomu msimu huu katika Serie A Andersson amesema lazima Ibrahimovic aoneshe kweli anataka kurejea kikosini, ili aweze kupanga kikosi kuelekea Euro 2020.

“Kwanza ni muhimu kwamba yeye mwenyewe kuhusika katika mradi wa timu ya taifa,” Andersson aliiambia Aftonbladet. Mwaka 2016 aliniambia kuwa hataki kuwa sehemu ya timu.

“Niliheshimu maamuzi yake na ni muda mrefu umepita, yeye ndiye anatakiwa kusema kuwa anataka kurejea katika kikosi, kisha baada ya hapo kazi itabaki kuwa kwangu mimi kuamua.”

Ibrahimovic ndiyo mfungaji bora wa muda wote wa timu ya Sweden akiwa amefunga magoli 62 katika michezo 116 lakini hajaichezea Nordic tangu wapoteze kwa 1-0 dhidi ya Belgium katika mashindano ya Euro mwaka 2016.

Andersson aliuliza kama mchezaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain na Manchetsr United kama yupo siriasi kuhusu kurejea katika timu ya taifa.

“Hatuja onana kwa muda mrefu,” alisema Andersson.”Sijamfuata katika mitandao yake ya kijamii lakini mimi sijali lolote kuhusu anachokisema huko.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

24 MAONI

  1. Ibrahimovic kwa sasa hana mda mrefu kwenye soka umri umeshaenda sana labda huenda hana ushirikiano na timu yake ya taifa labda anajua hata itumikia kwa mda mrefu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa