Ajax imekataa dau la Manchester United la pauni milioni 76.3 (€90m) kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Brazil Antony, winga huyo alifanya kazi na Erik Ten Hag wakati huo akiwa na Ajax, mazungumzo bado yanaendelea kati ya vilabu viwili kabla ya dirisha kufungwa.

antony, Antony Kwenda Man Utd: Ajax Wameikataa Ofa ya United., Meridianbet

United imekuwa ikimwinda mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa wiki kadhaa na kutoa ofa ya £67.9m sawa na paundi €80m ikikataliwa na klabu hiyo mapema wiki hii.

Antony aliondolewa kwenye kikosi cha Ajax kilichoshinda 1-0 Jumapili iliyopita dhidi ya Sparta Rotterdam, hivi karibuni mchezaji huyo ameonesha nia yake ya kutaka kuhamia Old Trafford, lakini mabingwa hao wa Eredivisie wamesimama kidete kupinga ofa iliyoboreshwa ya United.

“Tangu Februari mwaka huu, mawakala wangu walikuja Amsterdam kuwajulisha Ajax kuhusu nia yangu ya kuondoka kwenye klabu ili kukabiliana na changamoto mpya na kwamba baadhi ya vilabu vinavyovutiwa vitawasili na ofa nzuri,” Antony alisema kupitia mwandishi wa habari wa Italia. Fabrizio Romano kwenye YouTube.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa