Klabu ya Fulham inayoshiriki Ligi Kuu England imemtangaza rasmi aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa, kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Arbeloa mwenye umri wa miaka 43, ambaye pia aliwahi kuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa taji la Dunia mwaka 2010, anachukua nafasi ya Marco Silva aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita na kujiunga na Benfica ya Ureno.
Katika taarifa rasmi, Fulham ilieleza kufurahishwa na uteuzi huo ikisema: “Klabu inafuraha kutangaza uteuzi wa Alvaro Arbeloa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Fulham.” Arbeloa anarejea England akiwa na uzoefu wa awali wa kuchezea Liverpool, huku akiwa pia na mafanikio makubwa alipokuwa mchezaji wa Real Madrid ambapo alitwaa mataji mawili ya UEFA Champions League.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza baada ya uteuzi wake, Arbeloa alisema: “Ni heshima kubwa kwangu kuanza hatua hii mpya katika Fulham FC, klabu kongwe zaidi jijini London. Ninahisi wajibu mkubwa na niko tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuifikisha timu katika kiwango bora.”
Hata hivyo, safari yake ya ukocha katika Real Madrid haikuwa ya mafanikio makubwa. Baada ya kuchukua mikoba ya Xabi Alonso mwezi Januari mwaka huu, Arbeloa alishuhudia Real Madrid ikitolewa mapema katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Mfalme dhidi ya Albacete ya daraja la pili, huku ikipoteza nafasi ya kutwaa ubingwa wa La Liga kutokana na matokeo mabaya na pia kuondolewa na Bayern Munich katika robo fainali ya UEFA Champions League.
Marco Silva, ambaye sasa ni kocha wa Benfica, anaiacha Fulham baada ya kuiongoza kumaliza nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita. Sasa macho ya mashabiki yanaelekezwa kwa Arbeloa kuona kama ataweza kutumia uzoefu wake mkubwa wa soka kurejesha ushindani na mafanikio katika klabu hiyo ya London.


