Kiungo nyota wa Uturuki, Arda Güler, ameomba radhi kwa mashabiki wa taifa hilo kufuatia kuondolewa kwa timu yao katika hatua ya makundi ya mashindano ya Dunia 2026. Güler alizungumza kwa masikitiko makubwa baada ya matokeo mabovu yaliyoifanya Uturuki kushindwa kutimiza matarajio ya wengi.
Akizungumzia kampeni ya timu hiyo, Güler alikiri kuwa kiwango walichoonyesha hakikufikia viwango vinavyotarajiwa kwa kikosi chenye wachezaji wanaocheza katika baadhi ya vilabu vikubwa duniani. “Tunaomba radhi, tunajisikia vibaya na tunaona aibu,” alisema nyota huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Güler alieleza kuwa kikosi cha Uturuki kilikuwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi lakini kilishindwa kuonyesha ubora wake ndani ya uwanja. “Sisi sote tunacheza kwenye vilabu vikubwa na tulipaswa kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano haya,” aliongeza.
Moja ya mambo yaliyomuumiza zaidi ni kushindwa kwa timu hiyo kufunga hata bao moja katika michezo miwili iliyocheza. Kijana huyo wa miaka 21 alisisitiza kuwa hali hiyo haiendani na hadhi ya timu ya taifa ya Uturuki kwenye mashindano makubwa kama michuano ya Dunia.
“Katika mechi mbili, hatujafunga goli hata moja na hili jambo sio zuri na halikubaliki,” alisema Güler. Kauli hiyo inaonyesha namna ambavyo wachezaji wa Uturuki walivyokatishwa tamaa na matokeo yao huku wakiahidi kujifunza kutokana na makosa hayo kwa ajili ya mashindano yajayo.


