Kocha wa Liverpool FC, Arne Slot, amesema ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Galatasaray umetuma ujumbe mzito kwa Paris Saint-Germain kuelekea robo fainali ya UEFA Champions League.
Liverpool walifuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 licha ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini, na sasa wanatarajiwa kukutana na mabingwa watetezi PSG katika hatua inayofuata ya mashindano hayo makubwa barani Ulaya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Slot alikumbushia kuwa msimu uliopita PSG waliwaondoa Liverpool kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya 16 bora, licha ya timu yake kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa marudiano uliochezwa Anfield.
Akizungumza baada ya ushindi huo, Slot alisema: “Hawajashusha kiwango chao. Ilikuwa vigumu kwao kuboresha zaidi, lakini wamekuwa bora sana hadi sasa. Hata hivyo, baada ya mechi ya leo sidhani kama watakuwa na hamu ya kukutana nasi tena.”
Aliongeza: “Tulichezewa sana ugenini msimu uliopita, lakini Anfield tulicheza vizuri sana ingawa tulipoteza kwa penalti. Hii inaonyesha namna tulivyoboreshwa sasa.”
Slot pia alimpongeza Mohamed Salah kwa kuonyesha uimara wa kisaikolojia licha ya kukosa penalti, akisema: “Inaonyesha nguvu yake ya akili. Alikosa penalti kabla ya mapumziko, lakini alirudi kipindi cha pili na kutoa pasi ya bao pamoja na kufunga kwa mtindo wake wa kawaida.”

