Kocha wa Liverpool FC, Arne Slot, amesema timu yake italazimika kuonyesha kiwango cha “kipekee sana” ili kufuta pengo la mabao 2-0 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya UEFA Champions League.
Liverpool wako kwenye hatari ya kutolewa kwa msimu wa pili mfululizo na PSG baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha katika mchezo wa kwanza uliochezwa Paris, ambapo hawakupiga hata shuti moja lililolenga lango. Slot alikiri kuwa wanahitaji kubadilika kwa kiasi kikubwa ili kupata matokeo mazuri Anfield.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tunajua tunahitaji kiwango cha kipekee ili kufuzu hatua inayofuata, lakini hilo ni jambo la kawaida unapocheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya,” alisema Slot. “Katika mechi 49 za nyumbani chini yangu, mara 36 tumefunga mabao mawili au zaidi. Hilo linatupa imani kuwa tunaweza kufanya kitu maalum.”
Hata hivyo, Slot alikiri kuwa PSG ni wapinzani tofauti na wenye nguvu zaidi, lakini bado anaamini timu yake ina uwezo wa kufanya comeback. “Ni kweli hatujacheza mechi zote hizo dhidi ya PSG, lakini wapinzani wetu wa Ligi Kuu na Champions League walikuwa na nguvu. Tunahitaji kuwa wa kipekee sana ili kufanikisha hilo,” aliongeza.
Kocha huyo pia anakabiliwa na presha kubwa kufuatia matokeo mabaya ya hivi karibuni, ikiwemo kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Manchester City katika FA Cup, pamoja na kupoteza mechi dhidi ya Brighton na PSG. Hata hivyo, ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham FC uliwapa nafuu ya muda.
Slot amesisitiza umuhimu wa kuanza mchezo kwa kasi na kushambulia mapema ili kurejesha matumaini ya kufuzu. “Tunacheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya, hivyo kazi ni ngumu lakini siyo haiwezekani. Tunapaswa kuanza kwa nguvu na kuhakikisha tunarudi kwenye mchezo. Bao linaweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo,” alihitimisha.


