Klabu ya Arsenal inaweza kuweka historia  nyingine leo  kama itashinda mchezo wake wa nne mfululizo  dhidi ya Fulham,  ambapo  itakuwa ni mara yake ya 5 kufanya hivyo katika histori yao ya mpira na ndani ya mara hizo nne alichukua ubingwa misimu mitatu.  

Alifanya hivyo msimu wa 1930/1931, 1947/1948, 2003/2004,  pamoja na 2004/2005 ambapo ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kushinda mfululizo mechi za mwanzo za ligi.

Arsenal Kuweka Historia Leo
Gabriel Jesus, Arsenal.

Ikumbukwe kuwa Arsenal msimu uliopita alianza vibaya msimu baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo za ligi na baadae kuanza kufanya vizuri na hatimaye kumaliza msimu akiwa nafasi ya tano ambayo inamruhusu kushiriki michuano ya Europa barani Ulaya msimu huu.

The Gunners ndio  vinara wa ligi mpaka sasa wakiwa na alama tisa kwenye michezo mitatu waliyocheza. Leo hii watawakaribisha Fulham ambao  wapo katika nafasi ya saba ya msimamo huku wakiwa wameshinda mchezo mmoja na sare mbili.

Aleksandar - Arsenal vs Fulham

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa