Arsenal, Liverpool Wabanwa Ligi kuu Uingereza

Vilabu vya Arsenal na Liverpool vimebanwa koo katika michezo yao ya ligi kuu ya Uingereza waliyocheza leo baada ya kujikuta wakidondosha alama katika michezo ambayo walicheza katika viwanja vyao vya nyumbani.

Arsenal wao wakiwa katika dimba la Emirates wamelazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Everton ambayo ilionekana kuhakikisha inapata alama moja katika mchezo huo, Vijana wa Mikel Arteta walionekana kupambana kwa kiwango kikubwa kuhakikisha wanapata alama zote tatu lakini mambo hayakwenda kama walivyotaka.

arsenal

Liverpool upande wao wanapaswa kupongezwa kutokana na namna walivyopambana kuipata sare yao kwani dakika ya 11 tu Andreas Pereira anaipatia Fulham bao la kuongoza ambapo dakika ya 17 beki Andy Robertson anaoneshwa kadi nyekundu na kutolewa, Huku Liverpool wakicheza pungufu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikua nyuma kwa bao moja.

Kipindi cha pili mapema tu dakika ya 47 Cody Gapko anapokea pasi safi ya Mohamed Salah na kuisawazishia Liverpool na ubao kusoma 1-1 mpaka pale Fulham walipopata bao la pili dakika ya 76 kupitia kwa Rodrigo Muniz, Ambapo walipishana dakika 10 tu kwani mnamo dakika ya 86 Diogo Dalot na vijana wa Arne Slot kupata alama moja licha ya kucheza pungufu.

Mpaka sasa Liverpool wanaongoza bado msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 36 wakicheza michezo 15 sawa na Chelsea waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 31, Huku Arsenal wao wamecheza michezo 16 wakifanikiwa kukusanya alama 30, Hivo Liverpool akifanikiwa kushinda mchezo wake wa kiporo dhidi ya Everton atakua amewaacha vijana wa Arteta kwa jumla ya alama tisa.

Acha ujumbe