Arsenal na Manchester City Zatamba Kwenye Kikosi Bora cha PFA 2025/26

Chama cha Wachezaji wa Soka la Kulipwa nchini England (PFA) kimetangaza Kikosi Bora cha Mwaka cha Ligi Kuu ya England (PFA Premier League Team of the Year) kwa msimu wa 2025/26, huku Arsenal na Manchester City zikitawala kwa idadi kubwa ya wachezaji waliochaguliwa.

 Arsenal na Manchester City Zatamba Kwenye Kikosi Bora cha PFA 2025/26Kipa wa Arsenal, David Raya, amechaguliwa kuwa golikipa bora wa msimu, huku safu ya ulinzi ikiwa na wachezaji Jurriën Timber, Gabriel Magalhães na William Saliba, wote kutoka Arsenal, pamoja na Nico O’Reilly wa Manchester City.

Katika eneo la kiungo, Bruno Fernandes wa Manchester United ameungana na Declan Rice wa Arsenal na Rayan Cherki wa Manchester City. Wachezaji hao wamepewa nafasi kutokana na mchango wao mkubwa katika timu zao katika msimu uliopita.

 Arsenal na Manchester City Zatamba Kwenye Kikosi Bora cha PFA 2025/26Kwa upande wa washambuliaji, Antoine Semenyo, ambaye alicheza Bournemouth kabla ya kuhamia Manchester City, ameingizwa kwenye kikosi hicho pamoja na Igor Thiago wa Brentford na mshambuliaji hatari wa Manchester City, Erling Haaland.

 Arsenal na Manchester City Zatamba Kwenye Kikosi Bora cha PFA 2025/26Kwa ujumla, Arsenal imewakilishwa na wachezaji watano, huku Manchester City ikiwa na wachezaji wanne, Manchester United mmoja, Bournemouth/Manchester City mmoja na Brentford mmoja. Uchaguzi huo unaonyesha kiwango bora cha wachezaji hao katika msimu wa 2025/26.

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.