Ana Andika Deo Mwanasoka. Imani yangu bado inaniambia kuwa Mikel Arteta ni kocha sahihi sana kwa Arsenal, imani yangu bado inaniambia kuwa Pierre Emerick Aubameyang ni mshambuliaji bora zaidi wa katikati ndani ya epl baada ya Harry Kane. Imani yangu bado inaniambia hivo.

Anachokikosa Mikel Arteta ni wanajeshi wa kumbebea silaha na kumshindia vita. Ramani aliyoichora ipo sawa ila wabebaji na wasomaji hawapo sawa. Fasihi tukiiweka kando, Arsenal ina wachezaji wa kawaida kuliko jina la Arsenal. Nikosolewe hapa.

Subiri kwanza, Naizungumzia Arsenal yenye mashabiki wengi kuliko Everton. Naizungumzia Gunners yenye jina kubwa kuliko Leicester City. Dunia inataka ifanye vizuri kuliko hizi timu, ila haitaki kutazama tofauti ya pande mbili. Ndiyo shida ya walimwengu.

 

arsenal, Arsenal ni Kubwa Kuliko Kikosi cha Mikel Arteta., Meridianbet

Niliwahi kuandika hapa, tofauti ya haraka iliyopo kati ya Arsenal ya Arteta na ya Emery ni ulinzi. Akiwa na wachezaji walewale, Arteta ameifanya Arsenal kuwa timu ngumu kuruhusu bao.

Kinachomgharimu ni upande wa pili wa uwanja, hawafungi kabisa. Kama Arsenal walivo wagumu kufungwa tofauti na mwanzo, ni wagumu pia kufunga tofauti na mwanzo.

Hili la kutokufunga linaletwa na nguvu kubwa wanayotumia kujilinda. Muda mwingi wanautumia kulinda na kumiliki mpira, hawatumii kushambulia. Mabao hayawezi kuja kama hushambulii na kupiga mpira golini.

Sehemu pekee ninayopishana na Mikel ni kwa Aubameyang. Nadhani hatengenezewi nafasi za kutosha. Nadhani hatumiki vema kama anavopaswa kutumika. Unampangaje Auba ashambulie kutoka pembeni? Si sawa, ndiyo maana amemrudisha katikati juzi.

Kuhusu kumtengenezea nafasi? Auba anahitaji timu ya kumtengenezea situation za ‘one on one’, anahitaji kiungo mjanja wa kumpa pasi nyingi za mwisho, yeye amalizie tu. Hii kazi anaiweza nani mwingine zaidi ya Mesut Ozil?


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

arsenal, Arsenal ni Kubwa Kuliko Kikosi cha Mikel Arteta., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

30 MAONI

  1. Arsenal hasaivi haitabiriki kwa ukweli yani kama timu pizani ikiwapa mwanya tu basi wajue wameumia arsenal wanaitumia nafasi zao za ishindi vizuri tu

  2. Hakuna njia nyingine zaidi ya Arteta kuwashawishi mabosi wa Arsenal kufanya usajili tena kwenye sehemu zenye upungufu mkubwa ili kuirudisha Arsenal kwenye ramani pia ikumbukwe kuwa Mzimu wa Ozil lazima utawasumbua Arsenal Arteta hakutakiwa kuingia kwenye mgogoro na Ozil bali alitakiwa ajaribu kumtumia sababu watu wengi tunaimani Ozil bado ananafasi ya kumalizia malizia soka lake.
    ^EK

  3. The gunner wamekuwah kwny msimu mbaya Sana katika kipind cha mechi za hivi karibu natumain arteta anawez kuimalisha kikos chake kwny dilisha dogo January

  4. Kinachomgharimu ni upande wa pili wa uwanja, hawafungi kabisa. Kama Arsenal walivo wagumu kufungwa tofauti na mwanzo, ni wagumu pia kufunga tofauti na mwanzo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa