Arsenal Yamnasa Kipa Illan Meslier Kutoka Leeds United

Arsenal imekamilisha usajili wa kipa raia wa Ufaransa, Illan Meslier, kutoka Leeds United kwa uhamisho wa bure, huku mchezaji huyo akisaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi. Meslier anatua Emirates baada ya kuitumikia Leeds kwa miaka saba.

Arsenal Yamnasa Kipa Illan Meslier Kutoka Leeds United Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 ameondoka Leeds akiwa ameichezea mechi 215 katika mashindano yote na kutunza nyavu mara 70. Alianza soka lake la kulipwa akiwa FC Lorient kabla ya kujiunga na Leeds kwa mkopo mwaka 2019, ambapo aliisaidia timu hiyo kupanda Ligi Kuu England kabla ya usajili wake kufanywa wa kudumu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya kutambulishwa rasmi, Meslier hakuweza kuficha furaha yake ya kutua Arsenal na kusema ni hatua kubwa katika maisha yake ya soka. “Nina furaha kubwa. Hii ni siku maalum kwangu kwa sababu nimejiunga na mabingwa. Kwangu, Arsenal ndiyo klabu kubwa zaidi nchini England, na ninajivunia kuwa sehemu ya familia hii,” alisema Meslier.

Arsenal Yamnasa Kipa Illan Meslier Kutoka Leeds United Kipa huyo amesema lengo lake ni kuisaidia Arsenal kurejea kwenye mafanikio makubwa kwa kutwaa mataji. “Siwezi kusubiri kuonyesha mapenzi yangu kwa nembo hii na kupigania mafanikio ya timu. Hii ni klabu inayostahili kushinda mataji mara kwa mara, na ninataka kuwa sehemu ya historia hiyo,” aliongeza.

Arsenal Yamnasa Kipa Illan Meslier Kutoka Leeds United Usajili wa Meslier unatajwa kuwa sehemu ya mipango ya kocha Mikel Arteta kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya, huku Arsenal ikitarajia uzoefu na uwezo wa kipa huyo kuongeza ushindani katika nafasi ya walinda mlango na kusaidia timu kufikia malengo yake ya kutwaa mataji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.