Arsenal Yapanga Usajili Mkubwa Baada Ya Kutwaa Ubingwa

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu England Arsenal wanadaiwa kuanza mipango ya kufanya usajili mwingine mkubwa katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kumaliza ukame wa miaka 22 bila ubingwa wa ligi hiyo.

Arsenal Yapanga Usajili Mkubwa Baada Ya Kutwaa UbingwaViongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na mmiliki Stan Kroenke pamoja na mwanawe Josh Kroenke walihudhuria sherehe za ubingwa katika Uwanja wa Selhurst Park, lakini taarifa zinaeleza kuwa tayari mipango ya kuijenga zaidi timu hiyo imeanza.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Arsenal inaamini mafanikio ya msimu huu si mwisho wa safari bali ni mwanzo wa kipindi kipya cha ubabe ndani ya soka la England chini ya kocha Mikel Arteta.

Arsenal Yapanga Usajili Mkubwa Baada Ya Kutwaa Ubingwa“Ndani ya klabu kuna imani kubwa kuwa hiki kikosi bado kina uwezo mkubwa zaidi. Lengo si kushinda ubingwa mara moja pekee, bali kutawala soka la England kwa muda mrefu,” zilieleza taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo.

Arsenal Yapanga Usajili Mkubwa Baada Ya Kutwaa UbingwaTaarifa zinaeleza kuwa Arsenal inalenga kusajili kiungo, beki wa pembeni pamoja na mshambuliaji wa kushoto, huku pia ikiwa tayari kusaka straika mpya endapo nafasi nzuri itajitokeza kwenye soko la usajili.

Arsenal Yapanga Usajili Mkubwa Baada Ya Kutwaa Ubingwa“Arsenal sasa inaamini inaweza kushindania wachezaji bora duniani. Klabu ipo tayari kutumia fedha tena kuhakikisha inaendelea kuwa mbele ya wapinzani wake,” iliongeza taarifa hiyo.

Arsenal Yapanga Usajili Mkubwa Baada Ya Kutwaa UbingwaWakati huo huo, kiungo Declan Rice anatarajiwa kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ambao unaweza kuongeza mshahara wake wa sasa na kumkaribisha kwenye kiwango cha mshahara wa nyota mwenzake Bukayo Saka ndani ya Arsenal.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.