Arsenal inatarajiwa kuongeza kasi ya mipango yake ya usajili mara baada ya Michuano ya Dunia kumalizika kwa wachezaji wa England na Argentina, huku Morgan Rogers na Julian Alvarez wakitajwa kuwa miongoni mwa malengo makuu ya kocha Mikel Arteta kwa ajili ya msimu ujao. Mechi ya nusu fainali kati ya England na Argentina inaonekana kuwa na athari si tu ndani ya uwanja, bali pia katika soko la usajili.
Kwa mujibu wa taarifa Arsenal bado inamthamini sana nyota wa Aston Villa, Morgan Rogers, ambaye anaonekana kuwa chaguo bora la kuimarisha safu ya ushambuliaji. Hata hivyo, Aston Villa haitakuwa tayari kumuachia kirahisi baada ya tayari kukubali kumpoteza Youri Tielemans, huku ikiaminika kuwa itahitaji dau kubwa linalozidi pauni milioni 120 ili kufikiria kuuza mchezaji huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa uamuzi wa Rogers unaweza kutegemea msimamo wake mwenyewe kuhusu kuondoka Aston Villa. “Arsenal haitajua kama kuna nafasi ya kumsajili Rogers hadi pale atakaporejea kutoka kwenye michuano ya Dunia na mazungumzo rasmi kuanza,” imeeleza taarifa hiyo.
Kwa upande wa Julian Alvarez, mazingira yanaonekana kuwa rahisi zaidi kutokana na taarifa kwamba mshambuliaji huyo anataka kuondoka Atletico Madrid. Ingawa Barcelona tayari imewasilisha ofa kubwa, Atletico Madrid haishtuki kumuuza kwa mpinzani wake wa moja kwa moja nchini Hispania, jambo linaloweza kuipa Arsenal nafasi nzuri ya kumsajili. Pia inaelezwa kuwa Alvarez anavutiwa na mwelekeo wa Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta.
Arsenal inaamini kuwa kumalizika kwa safari za England na Argentina kwenye michuano ya Dunia kutafungua mlango wa mazungumzo rasmi kwa nyota hao wawili. Hata hivyo, gharama kubwa za usajili wa Rogers na Alvarez zinamaanisha uongozi wa klabu hiyo utalazimika kufanya maamuzi makini kabla ya kuwasilisha ofa rasmi katika dirisha hili la usajili.


