Kikosi cha Arsenal kimeanza safari jioni kuelekea jijini Budapest, Hungary, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG).
Mchezo huo mkubwa unatarajiwa kuchezwa Jumamosi, Mei 30, 2026 huku timu hizo mbili zikisaka kutwaa taji kubwa zaidi la vilabu barani Ulaya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
The Gunners wanaingia katika mchezo huo wakiwa na matumaini makubwa ya kuandika historia mpya chini ya kocha Mikel Arteta, ambaye ameiongoza timu hiyo kuwa na msimu bora katika mashindano ya ndani na kimataifa na kutwa kombe la EPL mimu huu. Arsenal imeonyesha kiwango bora tangu hatua za makundi hadi kutinga fainali hiyo kwa ushindi wa kuvutia mbele ya vigogo mbalimbali wa Ulaya.
“Tumefanya kazi kubwa kufika hapa na sasa tunataka kumalizia safari yetu kwa ushindi,” kilieleza chanzo kutoka ndani ya kikosi hicho wakati timu hiyo ikiondoka kuelekea Hungary kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa kihistoria.
Kwa upande wa PSG, matajiri hao wa soka la Ufaransa nao wanaingia kwenye pambano hilo wakitetea taji lao lao la UEFA Champions League baada ya miaka kadhaa ya uwekezaji mkubwa ndani ya kikosi chao. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili.
Mashabiki wa Arsenal duniani kote wameendelea kuonyesha matumaini makubwa kuelekea mchezo huo, wakiamini timu yao inaweza kurejea England ikiwa na “ndoo” ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. Fainali hiyo pia inatajwa kuwa moja ya mechi zinazovutia zaidi katika kalenda ya soka duniani mwaka huu.


