Arteta Amtetea KEPA Baada ya Makosa Katika Fainali ya Carabao CUP

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ametetea uamuzi wake wa kumchezesha kipa Kepa Arrizabalaga licha ya kufanya kosa kubwa lililoigharimu Arsenal kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City katika fainali ya Kombe la Ligi England (EFL Cup) iliyochezwa jana Jumapili kwenye dimba la Wembley.

Arteta Amtetea KEPA Baada ya Makosa Katika Fainali ya Carabao CUPKepa alifanya kosa la wazi kipindi cha pili baada ya kushindwa kuudhibiti mpira wa krosi uliopigwa na Rayan Cherki, hali iliyompa nafasi Nico O’Reilly kufunga bao la kwanza kwa kichwa. Dakika nne baadaye, O’Reilly alifunga tena na kuhitimisha matumaini ya Arsenal kurejea mchezoni.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Arteta Amtetea KEPA Baada ya Makosa Katika Fainali ya Carabao CUPArteta aliamua kumbakiza Kepa golini badala ya kipa namba moja David Raya kwa sababu alikuwa amecheza mechi zote za mashindano hayo msimu huu. Hata hivyo, uamuzi huo uligeuka kuwa pigo kwa timu hiyo baada ya makosa ya kipa huyo kugharimu matokeo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Arteta alisema “Naelewa lawama, lakini lazima nifanye kilicho sahihi na cha haki. Kepa alicheza mashindano yote, hivyo ingekuwa si haki kumbadilisha. Makosa ni sehemu ya mpira, na bahati mbaya yametokea wakati muhimu.”

Arteta Amtetea KEPA Baada ya Makosa Katika Fainali ya Carabao CUPKocha huyo aliongeza kuwa “Tunasikitika sana, ni matokeo magumu kuyakubali. Tulijua umuhimu wa mechi hii na tulitaka kushinda, lakini hatukufanikiwa. Kipindi cha kwanza tulikuwa bora na tulipata nafasi kubwa ambayo ingebadilisha mchezo.”

Arteta Amtetea KEPA Baada ya Makosa Katika Fainali ya Carabao CUPLicha ya kuongoza msimamo wa Premier League kwa tofauti ya pointi tisa, Arsenal imeshindwa kuongeza taji jingine tangu walipotwaa FA Cup mwaka 2020, huku matumaini yao ya kutwaa mataji manne msimu huu yakizimika baada ya kupoteza fainali hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.