Kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, amepuuza tetesi zinazoendelea kuhusu kuongeza mkataba mpya klabuni hapo, akisisitiza kuwa kwa sasa akili yake yote ipo kwenye mechi na malengo ya msimu huu. Kauli hiyo ameitoa kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth utakaochezwa Jumamosi.
Ripoti kutoka vyombo vya habari vya Uingereza zimeeleza kuwa Arsenal tayari imeanza mazungumzo ya awali na Arteta kuhusu kuongeza mkataba wake unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao. Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa si wakati sahihi wa kujadili hilo akisema “Hakuna taarifa yoyote kuhusu hilo. Hatuna muda wa kujadili kwa sasa.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Arteta aliendelea kuweka wazi msimamo wake kwa kueleza dhamira yake kwa klabu hiyo, akisema “Mwelekeo wote ni kwenye kile tunachopaswa kufanya hadi mwisho wa msimu. Nimejitoa kikamilifu hapa, nina furaha na najisikia vizuri. Familia yangu iko sawa, na bado nina malengo makubwa ya kutimiza hapa.”
Kwa upande wa kikosi, nyota wa Crystal Palace, Eberechi Eze, amerejea mazoezini Alhamisi baada ya kupona majeraha na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi katika mchezo huo. Hata hivyo, Arteta hakutoa taarifa kamili kuhusu hali za majeruhi wengine akiwemo Martin Odegaard, Bukayo Saka, Piero Hincapie, Riccardo Calafiori na Jurrien Timber.


