Mikel Arteta amekiri kwamba Arsenal wanahitaji kudhibiti hisia zao zaidi baada ya kukabiliwa na mashtaka mfululizo ya FA.

The Gunners walitozwa faini ya pauni 40,000 siku ya jana kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao katika sare ya bila kufungana dhidi ya Newcastle United, kufuatia rufaa ya kutaka penalti ya dakika za mwisho kwenye Uwanja wa Emirates.
Shitaka lingine likaja kwa upande wa Arteta kwa kukata rufaa sawa katika ushindi wa raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Oxford United, huku tabia ya Arsenal katika mechi zote mbili ikivutia ukosoaji.
Mchezo wa kesho wa derby ya London kaskazini dhidi ya Tottenham utatoa mtihani mwingine wa uwezo wa Arsenal kudhibiti hasira zao, huku wakitafuta kudumisha nafasi yao kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Arteta alikabiliwa na maswali kuhusu mashtaka katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi, ingawa alikiri timu inahitaji kufanya vyema katika kipengele hicho, anahisi hawezi kudhibiti hisia zake mwenyewe.
Kocha huyo amesema; “Ninajali sana sifa ya klabu, hasa yangu, siwezi kudhibiti. Mimi ni nani. Ninajaribu kufanya niwezavyo kuwatetea wachezaji, kutetea klabu na hiyo inakuja kwa watu fulani ambao hawataipenda. Kwa hakika, ikiwa kila mtu angependa, haitakuwa nzuri sana.”
Arteta amesema kwamba sio kwamba hajali ila anajali sana hasa anapofanya kazi zake, akiwa amekaa nyumbani huwa anajali mke wake anawaza nini na watu wanawaza nini lakini wao hawajui.

“Ninakubali kwamba tunapaswa kudhibiti kile tunachoweza kudhibiti na kuna mambo fulani ambayo tunaweza kufanya vizuri zaidi.”
Anamaliza kwa kusema kutokana na adhabu hiyo watakuwa wamejifunza na watajaribu kufanya hivyo, lakini katika ligi hii, hakuna hakikisho kwa sababu mchezo unaofuata utakuwa wa ushindani.


