Arteta Athibitisha Ødegaard Kukosa Mechi ya Leverkusen

Kocha mkuu wa Arsenal FC, Mikel Arteta, amethibitisha kuwa nahodha wa timu hiyo Martin Ødegaard hatakuwepo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Bayer 04 Leverkusen utakaochezwa leo Jumatano. Hata hivyo, Arteta ametoa taarifa njema kwa kuthibitisha kuwa beki wa kati William Saliba yupo fiti na tayari kucheza katika mchezo huo muhimu.

Arteta Athibitisha Ødegaard Kukosa Mechi ya Leverkusen

William Saliba alikosa michezo miwili iliyopita ya Arsenal katika mashindano yote kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, lakini sasa amepona na anatarajiwa kurejea kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo. Kurejea kwake kunampa nafuu Arteta kuelekea pambano hilo gumu la Ulaya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, kutokuwepo kwa Martin Ødegaard kunaacha pengo kubwa katika eneo la kiungo kwa Arsenal, hasa upande wa ubunifu wa mashambulizi. Arteta pia alieleza kuwa Riccardo Calafiori na Leandro Trossard wanaweza kuwepo kwenye kikosi, ingawa uamuzi wa mwisho utafanyika karibu na muda wa mchezo.

Arteta Athibitisha Ødegaard Kukosa Mechi ya Leverkusen

Aidha, Arteta alithibitisha kuwa wachezaji muhimu akiwemo Gabriel Magalhães, Declan Rice na Martín Zubimendi wote wapo tayari kwa mchezo huo. Upatikanaji wao unaipa Arsenal nguvu zaidi katika kikosi kuelekea mechi hiyo muhimu ya Ulaya.

Arsenal iliondolewa katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, na hivyo kushindwa kufikia ndoto ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu. Akizungumzia uzoefu huo, Arteta alisema timu yake imejifunza mambo mengi kutokana na tukio hilo.

“Ndiyo, unajifunza mambo uliyofanya vizuri na pia yale unayopaswa kuboresha, Huu ni mpira wa miguu na lazima uonyeshe uwezo wako kesho usiku. Ligi ya Mabingwa inahusu siku ya mchezo na ndani ya siku hiyo kuna nyakati muhimu.”

Arteta Athibitisha Ødegaard Kukosa Mechi ya Leverkusen

Arsenal inaingia katika mchezo huo ikiwa kwenye kiwango kizuri baada ya kuifunga Mansfield Town FC mabao 2-1 mwishoni mwa wiki na kufuzu hatua ya robo fainali ya FA Cup. Ushindi huo umeibua mjadala kuhusu uwezekano wa timu hiyo kutwaa mataji manne msimu huu, huku Arsenal pia ikiongoza msimamo wa EPL.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.