Arteta: Hakuna Tatizo Kati ya David Luiz na Ceballos.

Mikel Arteta amesema kwamba “hakuna tatizo” kati ya wachezaji David Luiz na Dani Ceballos baada ya wawili hao kuripotiwa kutofautiana wakati wa mazoezi.

Meneja wa Arsenal Arteta amesisitiza “hakuna kitu kilichotokea” katika viwanja vya mazoezi vya Colney na aliamua kuipiga chini stori hiyo.

“Mazoezi ni ya ushindani sana mambo kama haya hutokea mara kwa mara,” Arteta aliongea nawaandishi siku ya Ijumaa.

“Na mambo hayo yaliisha haraka sana ndani ya timu, hakuna zaidi ya kuongea hakuna tatizo kati yao.

Alipoulizwa kama alishuhudia mkwaruzano huo, arteta aliongeza: “Nilipata picha mbaya nilikuwa kwa mbali ndiyo maana tunafanya mazoezi bila uwepo wa watu wengine.

Arteta alikabiliana na ishu nyingine ya kinidhamu baada ya mchezaji raia wa Brazil Willian kuweka picha yake katika mtandao Instagram akiwa Dubai.

Sheria za serikali ya United Kingdom haziruhusu mtu kusafiri kwenda taifa lingine isipokuwa kwa sababu maalumwakati huu wa kukabiliana na COVID-19.

Willian alijiunga na Arsenal akitokea klabu ya Chelsea kwa uhamisho huru lakini amekuwa akipambana kujitafuta kuwa kwenye fomu nzuri akiwa hajafanikiwa kufunga goli na kutoa asisti mbili katika michezo saba ya Premier League msimu huu.

Arteta alipuuza kuongelea swala la Willian kama amekiuka utaratibu wa klabu kwa kusafiri mapaka Dubai na je atatemwa kwenye mchezo wa Jumapili dhidi Leeds United.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

15 Komentara

    Ni vizuri Kama hamna tofauti

    Jibu

    Afadhali ikiwa hvyo

    Jibu

    Nice information

    Jibu

    Basi sawa inapendeza sana

    Jibu

    Niceupdate

    Jibu

    kama wamemaliza tofauti zao hakuna shida maisha ya soka yaendelee

    Jibu

    Kam wamemaliza tofauti Ni jambo zuri

    Jibu

    Bora zaidi

    Jibu

    Arteta ni kocha hanayejielewa yeye kama yeye hatayamliza ukingalia ni kweli kila sehemu wanapo kutana watu tofauti tofauti lazima mambo kama hayo yatokee

    Jibu

    Vizuri Sana Kama hipo hivyo

    Jibu

    Mpira hautaki ugomvi

    Jibu

    Ni jambo la maana

    Jibu

    IPO vizuri

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Ni vizuri kuelewana

    Jibu

Acha ujumbe