Aliyekuwa nahodha wa Manchester United na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya, Ashley Young ametangaza rasmi kuwa atastaafu soka mwishoni mwa msimu huu.
Beki huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 40, ambaye kwa sasa anaitumikia Ipswich Town, hajacheza tangu mwezi Januari, hali iliyochangia kufikia uamuzi huo muhimu katika maisha yake ya soka.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Young, ambaye pia aliwahi kuzichezea klabu za Aston Villa na Manchester United, amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata katika kipindi chake chote cha miaka 23 ya kucheza soka la kulipwa.
“Ninajivunia sana na ninashukuru kupata nafasi ya kufanikisha mengi katika maisha yangu ya soka. Si kawaida kukaa na kutafakari mambo haya ukiwa bado upo uwanjani, lakini kwa kweli nimeishi ndoto yangu kwa zaidi ya miaka 23,” alisema Young.
Aidha, nyota huyo ameongeza kuwa anatarajia kutumia muda wa wiki na miezi ijayo kutafakari maisha yake yajayo nje ya soka, huku akisisitiza kuwa bado ana malengo ya kuisaidia timu yake kabla ya msimu kumalizika.
“Ni wakati sasa wa kutafakari kile nilichofanikiwa na pia kuamua hatua inayofuata katika maisha yangu. Lakini kwa sasa, ninazingatia kikamilifu mechi ijayo ya Jumamosi na kusaidia klabu kufikia lengo letu la kurejea Ligi Kuu England,” aliongeza.


