Aston Villa Yamnasa Johan Manzambi, Yaipiku Newcastle Dakika za Mwisho

Klabu ya Aston Villa inadaiwa kuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo nyota wa Uswisi, Johan Manzambi, baada ya kuipiku Newcastle United ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kumsajili kufuatia kiwango chake bora kwenye michuano ya Dunia 2026.

Aston Villa Yamnasa Johan Manzambi, Yaipiku Newcastle Dakika za MwishoAwali Newcastle ilikuwa imefikia makubaliano na Freiburg ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa ada inayoripotiwa kufikia pauni milioni 52. Hata hivyo, pande hizo zilishindwa kufikia mwafaka kuhusu maslahi binafsi ya mchezaji, jambo lililofungua nafasi kwa Aston Villa kuingilia kati na kusonga mbele katika mazungumzo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Athletic, Aston Villa imeharakisha mchakato wa usajili wa Manzambi baada ya kiungo wake Amadou Onana kupata jeraha la kano za goti, ambalo linatarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Aston Villa Yamnasa Johan Manzambi, Yaipiku Newcastle Dakika za MwishoManzambi alivutia macho ya wengi kwenye michuano ya Dunia nchini Marekani, Kanada na Mexico baada ya kufunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao katika michezo minne aliyoichezea Uswisi, kabla ya safari yake kukatizwa na jeraha la goti.

Aston Villa Yamnasa Johan Manzambi, Yaipiku Newcastle Dakika za Mwisho“Aston Villa imeongeza kasi ya mazungumzo na sasa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Johan Manzambi, huku Newcastle ikikosa tena mmoja wa wachezaji wake waliokuwa vipaumbele baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya maslahi binafsi,” imeeleza ripoti ya The Athletic.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.