Nahodha wa klabu ya Aston Villa, John McGinn, amemualika Prince William kuungana na timu hiyo katika sherehe za ushindi wa Europa League baada ya kushuhudia wakiiadhibu Freiburg mabao 3-0 kwenye fainali iliyochezwa Jumatano usiku katika Uwanja wa Besiktas uliopo Istanbul.
Prince William ambaye ni shabiki mkubwa wa Aston Villa alikuwa sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia kikosi hicho cha kocha Unai Emery kikitwaa taji lao la kwanza kubwa ndani ya miaka 30 pamoja na kombe la kwanza la Ulaya baada ya miaka 44.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kabla ya mchezo huo kuanza, Prince William aliwatembelea wachezaji wa Aston Villa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo jambo lililomfanya McGinn kumkaribisha rasmi kwenye sherehe za ushindi baada ya mechi hiyo.
“Yeye ni mtu wa heshima sana. Alikuwepo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya mchezo kuanza. Ni shabiki mkubwa wa Aston Villa hivyo asingekosa mchezo huu,” alisema McGinn.
“Ni mtu wa kawaida sana. Ni jambo kubwa kuwa na sapoti yake na tunatumaini itaendelea. Labda usiku wa leo anaweza kunywa vinywaji kadhaa pamoja nasi na mwisho wa usiku atoe hata kadi yake ya benki kulipia,” aliongeza McGinn kwa utani.
Katika mchezo huo, mabao ya Youri Tielemans, Emiliano Buendía na Morgan Rogers yalitosha kuipa Aston Villa ushindi mkubwa na kutwaa taji lao muhimu la kwanza barani Ulaya tangu miaka 44 iliyopita.
Prince William pia alionekana akishangilia kwa furaha kubwa jukwaani huku akirekodi kwa simu yake ya mkononi wakati McGinn akiinyanyua rasmi kombe hilo katikati ya shamrashamra za mashabiki na fataki za ushindi.


