Mkurugenzi Mtendaji wa Atalanta, Luca Percassi, amekataa kuondoa uwezekano wa Éderson kuondoka majira ya kiangazi huku akihusishwa na Manchester United, lakini akasisitiza: “Hatuna ofa rasmi, ni ishara tu za awali za kuvutiwa naye.”
Atalanta “itafanyia tathmini” ofa zitakazowasilishwa kwa kiungo huyo wa Brazil, ambaye pia anahusishwa na Atlético Madrid.
“Mpaka leo, hatuna ofa yoyote rasmi, bali ni ishara tu za awali za kuvutiwa naye,” alisema Luca Percassi akizungumza na Sky Sport (kupitia SOS Fanta) kuhusu uwezekano wa Éderson kuondoka majira ya kiangazi.
“Mpaka msimu utakapomalizika, ni vigumu kwa klabu kuanza kufanya hatua rasmi. Tutapitia kila kitu kwa utulivu mkubwa na kwa wakati sahihi,” aliongeza kiongozi huyo wa Atalanta.
Éderson mwenye umri wa miaka 26, yupo kwenye msimu wake wa nne akiwa na Atalanta. Amefunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi 40 kwenye mashindano yote msimu huu, huku mkataba wake katika Gewiss Stadium ukitarajiwa kumalizika Juni 2027.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Italia, La Dea wanaweza kukubali kumuzaa kiungo huyo wa Brazil kwa kiasi cha karibu euro milioni 40.
Imeripotiwa kuwa Atalanta itamwajiri aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Juventus na Napoli, Cristiano Giuntoli, kuwa mkurugenzi wao mpya wa michezo, akichukua nafasi ya Tony D’Amico msimu ujao.
Hata hivyo, Luca Percassi amekanusha kuwa Atalanta tayari imefikia makubaliano yoyote na Giuntoli.
“Cristiano Giuntoli ni mmoja wa viongozi bora katika soka la Italia ambaye amepata uzoefu katika ligi za chini. Tutaona kitakachotokea. Najua kwamba klabu nyingi zimewasiliana na Giuntoli; tutaona kama ni ‘ndoa’ ambayo tutaiingia.” Alisema Luca Percassi.
Atalanta iliifunga AC Milan mabao 3-2 ugenini Jumapili na ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa Serie A.