Klabu ya Atlético de Madrid imefikia makubaliano kamili ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Denmark, Morten Hjulmand, kutoka Sporting CP kwa ada ya jumla inayokadiriwa kufikia euro milioni 40 pamoja na nyongeza. Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Madrid kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha rasmi uhamisho wake.
Taarifa za usajili huo zimepewa nguvu na mtaalamu wa masuala ya uhamisho, Fabrizio Romano, ambaye ametangaza kauli yake maarufu ya “Here We Go” ikimaanisha kuwa dili hilo limefikia hatua ya mwisho. Atlético Madrid iliongeza juhudi katika mazungumzo ya siku za karibuni baada ya ofa yake ya awali kukataliwa na Sporting CP.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hjulmand, mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Sporting CP mwaka 2023 akitokea US Lecce na haraka akawa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi hicho. Kiungo huyo baadaye alipewa jukumu la kuwa nahodha wa timu hiyo kutokana na uwezo wake wa kuongoza na mchango wake mkubwa uwanjani.
Mchezaji huyo ambaye ameichezea timu ya taifa ya Denmark mara 27, anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya mipango ya kocha Diego Simeone kuelekea msimu wa 2026/27. Simeone amemtaka Hjulmand ili kuongeza nguvu, uimara na uwezo wa kudhibiti eneo la kiungo katika kikosi chake.
“Atlético Madrid imemchagua Hjulmand kama mhimili mpya wa safu yake ya kiungo, kutokana na uwezo wake wa kupambana na kuleta uwiano ndani ya timu,” ilieleza taarifa za karibu na klabu hiyo. Uhamisho huo bado unasubiri uthibitisho rasmi kutoka kwa klabu zote mbili, huku Hjulmand akitarajiwa kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya mara baada ya kukamilisha vipimo vya afya.


