Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Gabon na klabu ya Barcelona Pierre Emerick Aubameyang amevamiwa nyumbani kwake majira ya usiku hapo jana akiwa katika mapumziko, lakini yeye na familia yake wapo salama.

Aubameyang avamiwa kwake

Ripoti za polisi nchini Hispania wamesema kuwa inakadiriwa kuwa wanaume wanne walivamia nyumbani kwake kupitia bustani yake hiyo na kuanza kumtishia kwa kutumia silaha za moto,  chuma, Lakini pia hawakuishia hapo walimpiga pia.

Aubameyang ambae amekuwa akihusishwa kwenda Chelsea baada ya kuonekana kuwa hana nafasi katika kikosi cha Barcelona baada ya ujio wa Robert Lewandowski, Raphinha na wengine wengi. Timu hiyo kwasasa inanolewa na kocha mkuu  Xhavi Hernandes.

Aubameyang, Aubameyang Avamiwa Nyumbani Kwake., Meridianbet

Vilevile ni mechi chache tuu ambazo Aubameyang amecheza mpaka sasa klabuni hapo toka ajiunge nao  akitokea Arsenal ambao kwasasa ndio wanaongoza ligi kuu ya England kwenye msimamo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa