Hawapo nyuma sana na japo hawasemwi sana, lakini Azam FC wameendelea kukusanya pointi kwenye kila mchezo wa ligi kuu na jana walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo uliochezwa jana usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Feisal Salum Abdallah aliyefunga mabao mawili dakika ya tatu na 16, huku bao lingine likifungwa na beki wa kati wa Kimataifa wa Mali, Yoro Mamadou Diaby dakika ya 34.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 52, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wanaoongoza kwa pointi zao 60 wakifuatiwa na vigogo wenzao, Simba SC wenye pointi 58 baada ya timu hizo zote tatu kucheza mechi 25.

Wakati Azam FC wakifurahia ushindi huo, lakini hali ilikuwa tofauti kwa upande wa KMC kwani kufuatia kupoteza mchezo huo, wakibaki na pointi zao tisa baada ya kucheza mechi 25 pia hivyo kuendelea kushika mkia na kuonesha kila dalili kuwa hesabu za kuwepo kwenye ligi msimu ujao ni ngumu sana.


