Katika dirisha kubwa la usajili kuelekea msimu ujao, Azam wamefanikiwa kukamilisha usajili wa mastaa tisa wapya kuelekea msimu ujao ambao ni viungo, Issa Ndala, James Akamiko, Abdul Sopu, Cleophas Mkandala, Tape Edinho, mshambuliaji Kipre Junior, walinzi Nathan Chilambo, Malickou Ndoye na kipa Ali Ahmada.

Azam, Majembe ya Kimataifa Azam Mambo Safi, Meridianbet

Mpaka sasa ni mchezaji mmoja tu kati ya wale wa kimataifa waliosajiliwa ambaye bado hati yake ya uhamisho haijawasili.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith alisema: “Baada ya kuwa na mchezo wa kwanza wa kirafiki wiki iliyopita, kikosi chetu siku ya Jumamosi kilianza rasmi programu za wiki ya pili ya mazoezi ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao hapa El Gouna, Misri.

“Lakini habari nyingine njema kwa mashabiki wetu ni kuwa tayari tumekamilisha kupata hati za kusafiria za mastaa wetu wote wapya kutoka katika timu wanazozichezea isipokuwa, Malickou Ndoye ambaye naye hati yake ipo katika hatua za mwisho, hii yote ni katika kuhakikisha tunakuwa tayari na kamili kwa ajili ya msimu ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa