Baada ya Chelsea, Liam Rosenior Ahamishia Uzoefu Wake Paris FC

Kocha mpya wa Paris FC, Liam Rosenior, amesema uzoefu alioupata akiwa Chelsea utakuwa chachu ya mafanikio katika kazi yake mpya ya kuinoa klabu hiyo ya Ligue 1. Rosenior alizungumza hayo Alhamisi katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa Paris FC.

Baada ya Chelsea, Liam Rosenior Ahamishia Uzoefu Wake Paris FCRosenior mwenye umri wa miaka 42 aliteuliwa kuinoa Chelsea mwezi Januari, lakini alidumu kwa miezi michache pekee baada ya kuiongoza timu katika michezo 23 kabla ya kuachishwa kazi mwezi Aprili. Licha ya kipindi hicho kuwa kifupi, amesema kimekuwa na mafunzo mengi muhimu ambayo atayatumia katika hatua inayofuata ya maisha yake ya ukocha.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza kuhusu uzoefu wake Stamford Bridge, Rosenior alikiri kuwa kulikuwa na mambo ambayo angeweza kuyafanya vizuri zaidi, huku akisisitiza kuwa pia kulikuwa na mafanikio yaliyopatikana. Aidha, alieleza kuwa hana kinyongo na Chelsea wala mrithi wake, Xabi Alonso, na akamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya.

Baada ya Chelsea, Liam Rosenior Ahamishia Uzoefu Wake Paris FC“Tulijiunga na Chelsea katikati ya msimu na katika kipindi kigumu. Kuna mambo mengi niliyojifunza, mengine ningeyafanya vizuri zaidi na ninawajibika kwa hilo. Lakini pia kulikuwa na mambo mazuri tuliyofanya. Nitayabeba mafunzo hayo katika kazi yangu Paris FC na nina matumaini yataisaidia klabu hii kuwa miongoni mwa klabu kubwa duniani, alisema Rosenior.

Baada ya Chelsea, Liam Rosenior Ahamishia Uzoefu Wake Paris FCKocha huyo wa England pia alieleza kuwa alishawishika na maono makubwa ya Paris FC, akieleza kuwa Ligue 1 ni ligi yenye ushindani mkubwa na mradi wa klabu hiyo una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Paris FC, inayomilikiwa na kundi la kifahari la LVMH, ilimaliza katika nafasi ya 11 kwenye Ligue 1 msimu uliopita na sasa inalenga  kupiga hatua zaidi chini ya uongozi wa Rosenior.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.