Gareth Bale alifunga bao lake la 200 siku ya Alhamisi baada ya kuifungia Tottenham katika mechi ya Europa League dhidi ya LASK.

Bale Amefikisha Mabao 200 Katika Soka Lake.

Bale mchezaji wa kimataifa wa Wales alikuwa amekwamia kwenye mabao 199 kwa kilabu na nchi tangu alipoifunga Spurs katika ushindi wao wa 2-1 wa Ligi Kuu dhidi ya Brighton mwanzoni mwa Novemba.

Alikaribia kufikia hatua muhimu wakati Tottenham ilishinda 4-0 dhidi ya Ludogorets kwenye Ligi ya Uropa Novemba 26, lakini akafunga bao lake la 200 katika mechi ya Alhamisi kwenye mashindano ya Ulaya.

Bale aliweka historia kwa kufanikiwa kufunga goli ugenini tangu alipofunga hat-trick huko San Siro mwaka 2010 ambalo lilitokana na mkwaju wa penati, Bale akaisawazishia Spurs baada ya Peter Michorl kuweka LASK mbele.

Mchezaji huyo wa miaka 31 alifunga bao la kwanza kati ya mabao 167 ya kilabu kwa Southampton dhidi ya Derby Count mwezi Agosti 2006, wakati alipoifungia Wales kwa mara ya kwanza mwezi oktoba mwaka huo huo dhidi ya Slovakia.

Bale alijiunga tena na Spurs kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja kutoka kwa Real Madrid.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Bale, Bale Amefikisha Mabao 200 Katika Soka Lake., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

24 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa