UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kiungo wao wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda anatarajiwa kuwa miongoni mwa mastaa wa timu hiyo ambao wataanza kambi ya wiki nne ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’ mara baada ya kukamilisha majukumu ya timu ya Taifa.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka nchini leo Alhamisi kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi yao ya kabla ya msimu ‘Preseason’ ambapo wataweka kambi kwenye mji wa Ismailia kabla ya kurejea nchini Agosti 5, mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya tamasha la Simba day.

Banda alikuwa na majukumu ya timu ya Taifa iliyokuwa kwenye mashindano ya mashirikisho ya nchi za Kusini mwa Afrika ambayo yanaendelea nchini Afrika Kusini, ambapo staa huyo aliisaidia Malawei kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B.

Ahmed alisema: “Kama ambavyo tuliweka wazi kuwa tunatarajia kuondoka nchini kesho (leo), Alhamisi kwa ajili ya kambi yetu ya kabla ya msimu ambayo itakuwa katika mji wa Ismailia nchini Misri ambapo kambi hii itakuwa ya kipindi kisichopungua wiki nne mpaka mwanzoni mwa mwezi wa nane.

“Kambi hii itahusisha wachezaji wote wa kikosi chetu isipokuwa wale ambao wana majukumu ya timu za Mataifa yao, lakini pia tunatareajia kiungo wetu Peter Banda naye ataripoti mapema kambini na kuongeza mzuka wa kimataifa akitokea kwenye mashindano ya COSAFA.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa