Barcelona wameichagua Roma katika mchezo wa kuwania taji la Joan Gamper mwaka huu 2022 ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti 6 ilitangazwa siku ya Jumatano.

Barcelona Kumenyana na Roma Kombe la Joan Gamper

Mwaka jana Barca walichuana na Juventus ambapo pia kwa mara ya kwanza timu za wanawake zilihusishwa ambapo Barcelona walitwaa taji hilo kwa kuinyuka Juventus 3-0.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Roma kushiriki taji la Joan Gamper kwani mwaka 2015 walicheza dhidi ya Barca ambapo Barcelona walishinda kwa mabao 3-0 ingawa kwa upande wa timu yas wanawake itakuwa mara ya kwanza

Jose Mourinho ambaye anaifundisha Roma anarejea Camp Nou kukabiliana na timu ambayo aliwahi kuwa kocha msaidizi enzi za mwalimu Louis Van Gaal miaka 2000.

Ikumbukwe Mourinho alikabiliana mara kadhaa dhidi ya Blaugrana wakati akiinoa Real Madrid ambao ni wapinzani wakubwa nchini Hispania.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa