Wolves “Mbwa mwitu” wanajiandaa kuondoka kwa Ruben Neves. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 yuko katika miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake na gazeti la Mirror linaripoti kuwa, Barcelona watatoa ofa kwa mchezaji huyo wa Ureno ambayo inaweza kujumuisha makubaliano ya kubadilishana au mkopo na baadhi ya wachezaji wao wachanga.

 

Barcelona na Neves Mambo Mazuri

Wolves wanataka paundi milioni 50 kwa mtu ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Sergio Busquets, ambaye anaonekana kuondoka bila malipo.

Tayari vilabu vingi vya Uingereza vimeonesha nia ya kuitaka saini ya kiungo huyo, huku Arsenal, Manchester United na Manchester City wakiongoza mbio za kumnasa mchezaji huyo.

 

Barcelona na Neves Mambo Mazuri

Kocha wa Barcelona Xavi alikutana na viongozi na benchi la ufundi la timu hiyo na kuzungumza kuhusu kumhitaji kiungo huyo ambaye, anapewa nafasi kubwa ya kuziba nafasi ya Sergio Busquets pindi muda wake utakapoisha.

 

Barcelona na Neves Mambo Mazuri
Ruben Neves

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa