Mvutano mkubwa umeibuka kati ya Barcelona na Real Madrid baada ya rais wa Los Blancos, Florentino Perez, kutoa kauli kali kuhusu sakata la Negreira na kutangaza kuwa klabu yake itawasilisha jalada maalum UEFA dhidi ya Barcelona. Hatua hiyo imeifanya Barcelona kuanza kuchunguza uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya rais huyo wa Madrid.

Sakata la Negreira limeendelea kulitikisa soka la Hispania kwa miaka ya hivi karibuni baada ya kubainika kuwa Barcelona walifanya malipo kwa aliyekuwa makamu wa rais wa kamati ya waamuzi, Jose Maria Enriquez Negreira, kwa zaidi ya miaka 17. Ingawa Barcelona wamekuwa wakisisitiza kuwa malipo hayo yalikuwa kwa ajili ya ushauri na ripoti za waamuzi, Perez ameuita ufisadi mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya soka.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Perez alisema Real Madrid wameandaa jalada la kurasa 500 watakaloliwasilisha UEFA mwishoni mwa msimu ili suala hilo lichunguzwe kwa kina. Rais huyo alidai kuwa Real Madrid na timu nyingine nyingi zimekuwa zikiumizwa kwa miaka mingi huku Barcelona wakinufaika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Perez hakusimama hapo pekee, kwani aliishambulia pia La Liga na vyombo vya habari, akidai kuna mfumo unaoendelea kuifanyia Madrid vita. Kauli zake kali zimeongeza joto kwenye uhasama wa muda mrefu kati ya miamba hiyo miwili ya Hispania, huku mashabiki wa pande zote wakigawanyika kuhusu nani yuko sahihi.

Muda mfupi baada ya mkutano huo, Barcelona walitoa taarifa rasmi wakisema idara yao ya sheria inaanza kuchunguza hatua za kuchukua kutokana na madai na shutuma za Perez. Sasa sakata hili linaonekana kuhamia nje ya uwanja kabisa, likiwa si tu vita ya kisoka bali pia vita ya kisiasa na kisheria kati ya klabu mbili kubwa zaidi duniani.



