Klabu ya Barcelona imeifunga timu ya Inter Miami ya Major League Soccer kwa mabao sita bila majibu katika mchezo wa kirafiki wakati huu wa Pre-season wakiwa wanaendelea na ziara yao nchini Marekani.

Barcelona Yaigaraza Sita Nunge Inter Miami

Mabao ya Barca walifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye alifunga goli la ufunguzi dakika ya 19 ya mchezo dakika sita baadaye Raphinha akaweka bao la pili Ansu Fati akaweka bao namba tatu dakika ya 41 kabla ya kwenda mapumziko, dakika ya 55 Pablo Gavira akaiangamiza Miami bao la nne Depay akaongeza bao la tano dakika ya 69 wakati Dembele alihusika katika bao la sita dakika ya 70.

The Blaugrana wanapata ushindi huo mnono zikiwa kama salamu kwa mahasimu wao wa Laliga Real Madrid ambao watamenyana nao mchezo wa kirafiki siku ya Jumamosi .

Raphina akiwa mchezaji mpya kwenye kikosi cha Xavi hakusita kutuma salamu kwa Los Blanco kwa kudai kwamba Barca ni bora kuliko Real Madrid.

“Barcelona ni bora kuliko Real Madrid,” alisema Raphinha.


BASHIRI HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa