Barcelona wamekamilisha usajili wa beki wa kulia Sergino Dest akitokea klabu ya Ajax kwa dau la €21m.

Dest mwenye umri wa miaka 19 amepata umaarufu katika ligi ya Eredivisie msimu 2019-20 , kwa kuisadia timu ya Ajax kumaliza nafasi ya kwanza kabla ya ligi hiyo kukatishwa kufuatia kuzuka kwa janga la virusi vya Corona.

Kiwango hicho kilipelekea timu mbalimbali zikiwemo Barcelona na Bayern Munich kuhitaji huduma ya beki huyo wakati huu wa dirisha la usajili.

Mara ya kwanza Bayern walionekana kuwa katika mazungumzo makubwa na Ajax, na ripoti zikidai kwamba Bavaria hawajafikia makubaliano na Ajax wala Dest.

Barcelona Yaipiku Bayern Munich Kumnasa Dest.
Mchezaji Sergino Dest.

Lakini Barcelona wamefanikiwa kumnasa kinda huyo kwa dau la €21m (£19m/$25m) dau kubwa kuliko lile la Bayern Munich.

Taarifa kutoka kwa miamba ya LaLiga kupitia tovuti rasmi ya klabu: ” FC Barcelona na Ajax wamefikia makubaliano ya uhamisho wa Sergino Dest.

“Mchezaji atasaini tena mkataba baada ya misimu mitano, mwishoni mwa msimu 2024-25.

“Sergino Dest ana viwango vyote vinavyohitajika katika safu ya ulinzi: Anashambullia inapohitajika ni mtu mwenye ubunifu.

Dest ametua Camp Nou kuziba nafasi iliyoachwa na beki wa kulia Semedo ambaye ametimkia katika klabu ya Wolves.

Dest ni mzaliwa wa Uholanzi lakini ameamua kufuata Upande wa baba yake U.S.A na aliiwakilisha United State, U-17 na U-20 kabla hajacheza mchezo wake wa kwanza na timu ya wakubwa Setemba 2019 dhidi ya Mexico.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

43 MAONI

  1. Sergino Dest ana viwango vyote vinavyohitajika katika safu ya ulinzi: Anashambullia inapohitajika ni mtu mwenye ubunifu.

  2. Dest ni noma ya wachezaj wazur Sana kwny kikos cha Ajax natumain atakuwep namwendelezo mzuri hata kwny timu ya me mpya ya Barcelona

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa