Mshambuliaji wa Ufaransa, Bradley Barcola, amesema kikosi chake kinaamini kina uwezo wa kuivunja safu imara ya ulinzi ya Paraguay watakapokutana katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Dunia utakaochezwa Jumamosi. Amesema ushirikiano mzuri wa washambuliaji wa Ufaransa ndiyo silaha kubwa ya timu hiyo.
Ufaransa imekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa mashindano, ikishinda mechi zote nne ilizocheza, kufunga mabao 13 na kuruhusu mawili pekee. Nahodha Kylian Mbappé, Ousmane Dembélé na Bradley Barcola wamechangia mabao 12 kati ya hayo, wakiongoza safu ya ushambuliaji yenye makali makubwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tunafurahia sana namna tunavyocheza. Tunashambulia, tunapasia na tunalinda kama timu moja. Kucheza pamoja na wachezaji wa kiwango hiki ni jambo la kufurahisha sana,” amesema Barcola.
Barcola amesema wanatarajia mchezo mgumu dhidi ya Paraguay, ambayo iliwashangaza wengi kwa kuwaondoa mabingwa mara nne wa dunia, Ujerumani, kwa mikwaju ya penalti. Amesisitiza kuwa Ufaransa italazimika kutafuta mbinu tofauti ili kuvunja ukuta wa wapinzani wao.
“Tunajua haitakuwa rahisi kwa sababu Paraguay wanacheza kwa kujilinda sana. Tutatafuta njia mbadala za kuwafungua na tunaamini mfumo wetu utaendelea kufanya kazi hadi mwisho wa mashindano,” amesema Barcola. Pia ameeleza kuwa licha ya joto kali linalotarajiwa mjini Philadelphia, kikosi cha Ufaransa kimezoea hali hiyo baada ya kucheza kwa wiki kadhaa nchini Marekani.


