Bayern Wamng’ang’ania Gordon Licha Ya Bei Kufika €90m

Bayern Munich wameonyesha wazi hawapo tayari kuachana na nia ya kumsajili winga hatari wa Newcastle, Anthony Gordon, huku wakipanga kuimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu ujao. Hata hivyo, dili hilo limekwama kwenye suala moja kubwa, bei. Newcastle wameweka thamani kubwa inayofikia euro milioni 90, kitu ambacho kimezua mvutano mkali.

Bayern Wamng’ang’ania Gordon Licha Ya Bei Kufika €90m

Tayari mabingwa hao wa Ujerumani wameanza mawasiliano na upande wa mchezaji, wakionesha nia ya dhati ya kumpeleka Allianz Arena. Gordon ameibuka kuwa chaguo la juu kwenye mipango ya Bayern, wakimwona kama mchezaji mwenye kasi, ubunifu na uwezo wa kubadilisha mchezo, kile ambacho wanahitaji kwa sasa kwenye maeneo ya pembeni.

Kwa mujibu wa taarifa, Bayern wako tayari kumpa Gordon mkataba wa miaka mitano wenye maslahi makubwa, ishara kwamba wako tayari kumshawishi aondoke England. Mchezaji huyo mwenye miaka 25 amekuwa na msimu bora akiwa Newcastle, akihusika moja kwa moja kwenye mabao 22 (17 magoli na asisti 5), jambo lililomfanya kuwa bidhaa adimu sokoni.

Bayern Wamng’ang’ania Gordon Licha Ya Bei Kufika €90m

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lakini upande wa Newcastle nao hawako tayari kulegeza msimamo. Wakiwa chini ya presha ya sheria za kifedha (PSR), wanahitaji mapato makubwa, lakini hawataki kuuza kirahisi mmoja wa nyota wao muhimu. Bei ya €90M imewekwa si tu kwa ubora wake, bali pia kulinda maslahi ya klabu.

Bayern Wamng’ang’ania Gordon Licha Ya Bei Kufika €90m

Wakati klabu zikivutana, Gordon mwenyewe anaonekana kuwa tayari kwa changamoto mpya. Inasemekana yuko tayari kuhamia Ujerumani na kuvutiwa na nafasi ya kucheza Champions League na kupigania mataji makubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.