Kiungo wa England, Jude Bellingham, amesema ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico uliowavusha Three Lions hadi robo fainali ya mashinano ya Dunia ni usiku bora zaidi katika maisha yake ya kuitumikia timu ya taifa. Nyota huyo wa Real Madrid alifunga mabao mawili ndani ya sekunde 95 kipindi cha kwanza na kuzima matumaini ya mashabiki zaidi ya 80,000 waliofurika Uwanja wa Estadio Azteca.
Licha ya kuongoza mchezo, England ililazimika kupambana kwa sehemu kubwa ya kipindi cha pili ikiwa na wachezaji 10 baada ya Jarell Quansah kutolewa kwa kadi nyekundu. Bao la penalti la Harry Kane liliihakikishia England ushindi muhimu ambao umeiwezesha kupanga miadi na Norway ya Erling Haaland katika hatua ya robo fainali.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Huu ndio usiku bora zaidi katika maisha yangu ya kuichezea England. Siwezi hata kuelezea ninavyojisikia kwa sasa. Kulikuwa na mabao, penalti kwa pande zote mbili na kadi nyekundu. Ilikuwa mechi ya vurugu nyingi, lakini timu yetu ilionyesha moyo mkubwa wa kupambana na ninajivunia kila mmoja,” alisema Bellingham.
Bellingham pia aliisifu timu kwa namna ilivyokabiliana na presha kubwa, kucheza kwenye mwinuko mkubwa na kuchelewa kwa mchezo kutokana na hali mbaya ya hewa. Alisema kizazi cha sasa cha England kimeonyesha tofauti kubwa na timu alizokuwa akizishabikia alipokuwa mtoto.
“Miaka ya nyuma England ingeweza kuporomoka katika mazingira kama haya, lakini safari hii tulisimama pamoja hadi filimbi ya mwisho. Ndoto yangu ni kuiunganisha nchi yangu kupitia soka na kuwapa Waingereza usiku wa furaha kama huu. Ninajivunia sana kile tulichokifanya leo,” aliongeza Bellingham.


