Klabu ya Benfica ya Ureno imetangaza rasmi kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Jhon Durán, kwa mkopo kutoka Al Nassr ya Saudi Arabia. Makubaliano hayo yanajumuisha kipengele cha kumnunua moja kwa moja endapo masharti yaliyowekwa kwenye mkataba yatatimizwa, huku ada ya uhamisho wa kudumu ikitajwa kuwa takribani euro milioni 30.
Durán mwenye umri wa miaka 22 amekuwa na safari ya kipekee katika soka la kimataifa, akianza kung’ara kwenye Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kabla ya kuhamia Aston Villa ya England. Baadaye alijiunga na Al Nassr, lakini alishindwa kupata nafasi ya kudumu na kutolewa kwa mkopo Fenerbahçe katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2025/26, kabla ya kuhamia Zenit St. Petersburg kwa mkopo katika nusu ya pili ya msimu huo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Baada ya kukamilisha usajili wake, Durán hakuweza kuficha furaha yake ya kujiunga na mabingwa hao wa Ureno. “Nimejiunga na klabu kubwa zaidi nchini Ureno. Ni heshima kubwa kwangu kuvaa jezi ya Benfica, na nipo tayari kutoa kila kitu kwa ajili ya timu,” alisema mshambuliaji huyo.
Kwa upande wake, Benfica imeeleza kuwa usajili wa Durán ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya. “Tunamkaribisha Jhon Durán katika familia ya Benfica. Tunaamini ubora wake na uwezo wake wa kufunga mabao utaleta mchango mkubwa kwa timu,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.
Iwapo masharti ya mkataba wa mkopo yatatimizwa, Benfica itanunua rasmi huduma za mshambuliaji huyo kwa ada inayokadiriwa kufikia euro milioni 30. Mashabiki wa klabu hiyo sasa watakuwa na matarajio makubwa ya kumuona Durán akirejea kwenye kiwango chake bora akiwa nchini Ureno.


