Siku moja Bernard Morrison atafunga ukurasa wake kwenye soka la Tanzania, utachagua wewe umkumbuke BM3 kwa lipi, ila binafsi nitaikariri kurasa moja nzuri sana kutoka kwa Benny.
Bernard Morrison
Bernard Morrison

Kwenye kitabu chake ametupa somo zuri sana kuhusu mpira wa miguu kuwa ni AJIRA, yes kuna misamiati minne PROFESSION, PROFESSIONAL, PROFESSIONALSM na PROFESSIONALITY

Alipiga hela pale Msimbazi pasipokujali kelele za Yanga, pasipokujali mitaa itasemaje yeye aliwaza zaidi account zake za benki, akafika Simba na kufanya kazi yake iliyomleta nchini

Bernard Morrison alifahamu Simba ni tiketi yake eidha ya kurejea Yanga au kusalia kwa pesa nzuri zaidi, hakujali kuhusu kelele zenu, hakujali kuhusu mitaa bali alijali account zake za benk zinasemaje, hilo ndilo la msingi zaidi kwake
Bernard Morrison
Bernard Morrison

Zama za “Usihame mwanangu Mjomba atanuna” hizo zimepita, zile zama za “Hii timu yangu naipenda kutoka moyoni” zimepita hizo, wewe utazame mpira kama kazi, fanya kazi yako rudi nyumbani ukapumzike

Kujadili mikataba kishkaji, kujadili mikataba kwa kujuana kunawatoa nje ya dunia ya kibepari, mnaishije kwenye zama za Ujamaa kwenye ulimwengu wa vipande vya fedha?


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa