Viongozi wa timu ya Biashara United ya Mara wamejiuzulu baada ya timu hiyo kushuka daraja katika mkutano wa dharura uliofanyika juzi jumatatu.
Timu ya Biashara United imeshuka daraja moja kwa moja pamoja na timu ya Mbeya Kwanza na watashiriki michuano ya Championship kwa msimu ujao wa 2022/23.
Biashara, Viongozi Biashara United Wajiuzulu, Meridianbet
Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso, amesema kuwa “Tulifanya mkutano wa dharura na wanachama juzi jumatatu kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya klabu yetu.
“Hayakuwa malengo yangu timu kushuka daraja lakini pamoja na viongozi wenzangu tumeamua kupisha wengine ambao watachaguliwa ili tuweze kuwapa ushirikiano na timu irejee tena ligi kuu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa