Mchezaji wa Hertha Berlin ya Ujerumani inayoshiriki Bundesliga imetangaza kuwa mchezaji wa Jean Paul  Boetius anayecheza nafasi ya winga  atafanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa baada ya vipimo kubaini kuwa Mholanzi huyo ana uvimbe kwenye tezi dume.

 

Boetius Apata Tezi Dume

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, aliyecheza mara moja na Uholanzi, ni mchezaji wa zamani wa Feynoord na Basel ambaye alijiunga na Hertha Berlin mnamo Agosti baada ya kukaa na miaka minne na Mainz.

Klabu yake ilisema katika taarifa: “Jean Paul Boetius amagundulika kuwa na uvimbe kwenye tezi dume kufuatia matokeo ya uchunguzi wa mkojo siku ya Jumatano, na atakuwa nje kwa siku zijazo. Mchezaji huyo atafanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa..”

Fred Bobic ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa michezo wa Hertha Berlin, alimuunga mkono Boetius kupata ahueni kabisa. Bobic alisema; “Japokuwa ni vigumu kusikia mwanzoni, tumejaa matumaini kwamba Jean Paul atapata nafuu na kurejea kwetu haraka iwezekanavyo.

“Atapata msaada wetu kamili, hadi atakaporudi. Familia ya Hertha iko kando yake na inamtakia kila lakheri”

Habari kwa Boetius inafuatia mshambuliaji wa Borrusia Dortmund, Sebastian Haller kugundulika kuwa na uvimbe kwenye tezi dume mwezi Julai, wiki chache tuu baada ya kujiunga na Dortmund akitokea Ajax.

Boetius Apata Tezi Dume

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa