Klabu ya AFC Bournemouth imemwondoa beki wake Alex Jimenez kutoka kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Fulham FC kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusu ujumbe unaodaiwa kumhusisha na mtoto mwenye umri wa miaka 15.
Jimenez mwenye umri wa miaka 21 amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Bournemouth tangu Novemba ambapo amecheza karibu kila mchezo wa Premier League chini ya kocha Andoni Iraola. Hata hivyo, klabu hiyo imethibitisha kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Craven Cottage kwa mchezo wa Jumamosi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kupitia taarifa rasmi, Bournemouth ilisema “Klabu inafahamu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinazomhusisha Alex Jimenez. Tunaelewa uzito wa suala hili na kwa sasa linafanyiwa uchunguzi.”
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa kutokana na hali hiyo, mchezaji huyo hatajumuishwa kwenye kikosi cha mchezo dhidi ya Fulham huku klabu hiyo ikisisitiza kuwa haitatoa maoni zaidi kwa sasa hadi uchunguzi utakapokamilika.
Hatua hiyo imekuja baada ya kusambaa kwa picha za mazungumzo na video zinazodaiwa kuonyesha mawasiliano kati ya Jimenez na mtoto wa miaka 15, jambo lililoibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ndani na nje ya England.
Licha ya sintofahamu hiyo, Bournemouth wanaendelea kupigania nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao wakiwa katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi huku zikiwa zimebaki mechi tatu kabla ya msimu kumalizika.


