Brazil Yaibuka Kivingine, Haiti Yatupwa Nje ya Mashindano

Timu ya taifa ya Brazil imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Dunia la 2026 baada ya kuichapa Haiti mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi C uliochezwa kwenye Uwanja wa Lincoln Financial Field jijini Philadelphia. Matokeo hayo yameirejesha Brazil kwenye mbio za kusaka tiketi ya hatua inayofuata ya mashindano.

Brazil Yaibuka Kivingine, Haiti Yatupwa Nje ya MashindanoBrazil ilianza kuonyesha ubora wake mapema katika mchezo huo kupitia mshambuliaji Matheus Cunha aliyefunga mabao mawili ndani ya dakika saba. Cunha aliifungia Brazil bao la kwanza dakika ya 24 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 31 na kuiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kuondoka na alama tatu muhimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Wakati Haiti ikijaribu kujipanga upya, Vinícius Júnior aliongeza maumivu kwa kufunga bao la tatu katika dakika ya 45+3. Bao hilo lilihakikisha Brazil inaenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao matatu bila majibu na kudhibiti mchezo kwa kiasi kikubwa.

Brazil Yaibuka Kivingine, Haiti Yatupwa Nje ya Mashindano“Brazil ilionyesha ubora wake wa kawaida mbele ya lango,” huku Matheus Cunha akiwa nyota wa mchezo kwa mchango wake mkubwa wa mabao mawili. Ushindi huo umewapa Wabrazil nguvu mpya baada ya kuanza mashindano kwa matokeo yasiyoridhisha.

Brazil Yaibuka Kivingine, Haiti Yatupwa Nje ya MashindanoKwa upande wa Haiti, kipigo hicho kimekuwa pigo kubwa kwani kimeifanya kuwa timu ya kwanza kuondolewa rasmi katika mashindano ya Dunia 2026. Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, matumaini ya Haiti ya kusonga mbele yamefutika rasmi huku Brazil ikijiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania kufuzu hatua ya mtoano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.