Klabu ya Olympique Marseille imemtangaza rasmi Bruno Genesio kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Habib Beye, ambaye ameondoka baada ya kudumu kwa miezi minne pekee akiwa benchi la ufundi. Uteuzi huo umetangazwa Jumatano huku Genesio akitarajiwa kuanza kazi katika Uwanja wa Stade Vélodrome kuelekea msimu mpya wa Ligue 1.
Akizungumza baada ya kutambulishwa, Genesio alisema amevutiwa na changamoto mpya iliyopo Marseille pamoja na historia kubwa ya klabu hiyo. “Nimechagua kujiunga na Olympique Marseille kwa sababu nilivutiwa na changamoto iliyopo hapa. Hii ni klabu ya kipekee yenye historia kubwa, utambulisho imara na mashabiki wenye shauku inayotambulika duniani kote. Nina furaha kuwa sehemu ya mradi huu mpya,” alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 59.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Genesio anatua Marseille baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na Lille, ambapo alisimamia jumla ya mechi 99 katika mashindano yote. Msimu uliopita aliiongoza Lille kumaliza nafasi ya tatu katika Ligue 1, mafanikio yaliyoiwezesha klabu hiyo kufuzu kushiriki michuano ya UEFA Champions League.
Kabla ya hapo, Genesio aliwahi kuifundisha Lyon, ambako alisimamia mechi 185 na kuiongoza timu hiyo kufuzu mara mbili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Pia aliwahi kuwa kocha wa klabu ya Beijing Guoan nchini China na baadaye Rennes, ambako alifanya kazi kwa miaka miwili na kujijengea sifa kama mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa nchini Ufaransa.
Akiwa mchezaji wa zamani wa nafasi ya kiungo, Genesio alicheza zaidi ya mechi 200 katika ligi daraja la kwanza na la pili nchini Ufaransa kabla ya kuingia kwenye ukocha. Sasa anakabiliwa na jukumu la kuirejesha Marseille katika ushindani wa juu wa soka la Ufaransa na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Ulaya msimu ujao.


