Bruce Buck baada ya kuhudumu kwa miaka 19 katika nafasi ya Uenyeketi kwenye klabu ya Chelsea sasa ataachia nafasi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Tangu mwaka 2003 Buck amekuwa mwenyekiti wa The Blues wakati Roman Abramiovich alipoinunua klabu hiyo ya Premier League ambapo kipindi chote alifanikiwa kutwaa mataji 21 ambapo ni pamoja na mataji 5 ya EPL na Mawili ya Ligi ya Mabingwa.

Buck alitangaza kwamba ataachana na majukumu hayo na kuhamia kwenye majukumu ya ushauri wa klabu kuanzia Juni 30 lengo ni kumsaidia Boehly na timu yake kupata mafanikio makubwa.

“Najivunia kuisadia Chelsea kwenye mafanikio makubwa ndani ya uwanja na kuleta matokeo makubwa kwenye jamii.” alisema Buck.

“Sasa ni wakati wa kuachia nafasi hiyo na kuacha umiliki mpya kujenga msingi imara tuliyonao.

Boehly alisema: “Bruce ameipeleka Chelsea katika ngazi ya juu, tunamshukuru kwa huduma yake na kujitolea kwenye klabu.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa